Thursday, August 4, 2011

TENDWA ASIKITISHWA NA WABUNGE KUVURUGA VIKAO VYA BUNGE!

Msajili wa vyama vya siasa nchini Bwana JOHN TENDWA amesikitishwa na tabia ya baadhi ya wabunge kuvuruga utaratibu wa vikao vya bunge vinavyoendelea bungeni mjini Dodoma badala ya kufuata taratibu na kanuni za bunge

Msajili TENDWA amesema anashindwa kuchukua hatua zozote wakati vurugu hizo zinapotokea, kwa kuwa sheria haimruhusu kufanya hivyo.


Katika hatua nyingine ametoa wiki mbili kwa vyama vya siasa ambavyo havijarejesha ripoti zao na endapo vitashindwa kufanya hivyo vitapigwa faini ya Shilingi Milioni Tatu pamoja na kupoteza sifa za kushiriki katika uchaguzi wowote.

No comments:

Post a Comment