Thursday, August 4, 2011

KAMATI YA MIUNDOMBINU YAOMBA SEKTA YA RELI IPEWE KIPAUMBELE!

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imeiomba serikali kuipa kipaumbele na uhai sekta ya reli nchini kwani mafanikio ya bandari na ukuaji wa uchumi kwa kiasi kikubwa yanategemea mchango wa sekta hiyo.

Akiwasilisha mapendekezo ya Kamati ya Miundombinu bungeni Mwenyekiti wa kamati hiyo Mheshimiwa PETER SERUKAMBA amesema serikali ikiendelea na mwenendo uliopo taifa litaachwa nyumba kimaendeleo.


Utafiti uliofanywa na kamati hiyo umegundua kuwa nchi za Angola na Msumbiji zinajenga reli kwenda nchi zinazopakana nazo na hivyo kusababisha reli ya kati na Tazara kukosa mizigo ya kusafirisha.

No comments:

Post a Comment