Thursday, November 24, 2011

NEC YAMVUA UKATIBU ALIYEKUWA KATIBU WA CCM MKOA WA DSM KILUMBE NG’ENDA.!

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiendesha kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma leo. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) Amani Abeid Karume na kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Wilson Mukama.


Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi na Uenezi CCM, Nape NNauye akifuatilia kwa makini mijadala mbalimbali iliyokuwa ikiendelea katika mkitano wa NEC mjini Dodoma leo. Kulia ni Katibu wa NEC, Mambo ya Nje Januari Makamba.
Wajumbe wa NEC, Angella Kairuki na Anna Abdallah wakionyeshana mambo kwenye mtandao wakati wakiwa kwenye kikao cha NEC leo
Katibu wa NEC Oganaizesheni Asha Abdallah Juma akimsalimia Mjumbe wa NEC Andrew Chenge.
Mjumbe wa NEC, Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa na Kingunge Ngombale-Mwiru wakiwa katika kikao hicho leo.
Wajumbe wa NEC, Spika wa Bunge Anna Makinda na Abdulrahman Kinana wakitazama jarida la masuala ya siasa wakiwa kwenye kikao hicho.
Katibu wa NEC, Mambo ya Nje Januari Makamba na Katibu wa NEC Oganaizesheni Asha Abdallah Juma wakijadili jambo. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai
Mjumbe wa NEC na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Waziri Mkuu Mizengo Pinda akitoa ufafanuzi kuhusu jambo lililokuwa likijadiliwa katika kikao hicho.

Na Theeastafrica Bloger
Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM (NEC), imemvua nafasi ya Ukatibu, aliyekuwa katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam KILUMBE NG’ENDA.

Akizungumza na waandishi wa habari Mjini Dodoma ambako mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM unaendelea, Katibu wa CCM Itikadi na Unezi NAPE NNAUYE amesema KILUMBI NG’ENDA amevuliwa cheo hicho kwa kosa la kwenda kinyume na maamuzi ya vikao halali vya chama kwenye masuala ya uchaguzi wa madiwani wa viti maalum.


Wakati huo huo Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania JAKAYA KIKWETE kesho anatarajiwa kufungua semina ya siku tatu kwa watendaji wa CCM Taifa hadi ngazi ya wilaya inayohusu kujadili njia za kufanikisha shughuli za utendaji ndani ya Chama.


Katika hatua nyingine CCM tayari imeanza maandalizi ya uchaguzi mdogo wa Jimbo la Uzini Visiwani Zanzibar.

No comments:

Post a Comment