Jukwaa la Katiba nchini linatarajia kufanya maandamano makubwa ya amani nchi nzima Novemba 26 mwaka huu kwa madhumuni ya kumshauri Rais JAKAYA KIKWETE asiweke saini katika muswada wa mabadiliko ya Katiba mpya kwa sababu wananchi wengi wamekosa fursa ya kushiriki katika mchakato wa katiba kuanzia hatua ya awali kitendo ambacho kinaweza kusababisha kuundwa kwa katiba isiyokuwa na tija kwa wananchi.
Mwenyekiti wa Jukwaa hilo Bwana DEUS KIBAMBA amesema endapo Rais atasaini kuna hatari kubwa ya rasimu ya katiba itakayopatikana kukataliwa na wananchi huku matokeo yake yatakuwa ni kupoteza fedha nyingi za wananchi na kuendelea kutaabika kwa uamsikini.
Nae mjumbe wa Jukwaa la katiba nchini Bi ANANILEA NKYA amedai kuwa amesikitishwa na baadhi ya wabunge wanawake kwa vitendo vyao vya kukebehi na kubezana wao na vyama vyao wakati wa mjadala wa uundwaji wa katiba mpya ulivyokuwa ukijadiliwa Bungeni.
Maandamano hayo katika mkoa wa DSM yanatarajia kuanzia viwanja vya Mnazi mmoja hadi viwanja vya Jangwani.
No comments:
Post a Comment