Tuesday, December 20, 2011

KESI INAYOMKABILI MHARIRI MTENDAJI TANZANIA DAIMA YAHAIRISHWA HADI JANUARI 19,2012!

Kesi inayomkabili Mhariri Mtendaji wa gazeti la Tanzania Daima Bwana ABSOLOM KIBANDA imeahirishwa mpaka Januari 19, 2012 baada ya kusomwa kwa mara ya kwanza leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam.

Bwana Kibanda anakabiliwa na shitaka la uchochezi kufuatia habari iliyochapishwa na gazeti hilo iliyokuwa na kichwa cha habari kisemacho kuwa waraka maalumu kwa askari wote iliyoandikwa na SAMSON MWIGAMBA.


Mbele ya mahakama hiyo, Bwana KIBANDA amekanusha kuhusika na uchochezi, na ameachiliwa kwa dhamana. Mmoja wa mawakili wanaosimamaia kesi hiyo upande wa mshtakiwa, Bwana NYARONYO KICHEERE anafafanua.
                                                                     Nyaronyo Kicheere.

No comments:

Post a Comment