Thursday, October 27, 2011

MIILI YA MAREHEMU 12 WA AJALI YA BASI LA DELUX MISUGUSUGU KIBAHA WAZIKWA KWENYE MAKABURI YA AIR MSAE LEO!

 Baadhi ya viongozi wa dini mbalimbali walikuwepo kuendesha dua kwa miili ya marehemu kabla ya mazishi.
           Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza akiwa na Naibu Waziri wa Fedha George Gregori.

                      Baadhi ya majeneza yakiandaliwa kwa ajili ya kufanyiwa ibada/dua kabla ya mazishi
Baadhi ya ndugu na jamaa wa marehemu wakiwa katika maombelezo kutokana na majonzi makubwa ya kuondokewa na wapendwa wao.
        Ni wakati wa majonzi na simanzi kwa viongozi wa dini na wapendwa waliohudhuria dua hiyo.
Hilo ndilo eneo la Makaburi ya Msae ambalo miili ya marehemu 12 wa ajali ya basi la Delux imepumzika kwa amani.
Baadhi ya Makaburi yaliyopumzishwa wapendwa wetu wa ajali ya basi la Delux eneo la Misugusugu.
                                                             Hapa shughuli za mazishi zikiendelea
Baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki waliofika katika eneo la Makaburi kuwasindikiza wapendwa wao. Mungu azipumzishe roho za marehemu mahali pema peponi. Mbele yetu nyuma yao Bwana ametoa bwana ametwaa! Asante kwa mdau aliyetutumia picha hizi!

Na Theeastafrica Bloger
Miili ya marehemu 12 ya abiria waliopata ajali juzi katika basi la Kampuni ya Delux Coach iliyotokea katika eneo la MISUGUSUGU Wilayani KIBAHA wamezikwa leo katika makaburi ya Air Msae, Mjini KIBAHA.

Mazishi hayo ambayo yamehudhuriwa na umati wa wananchi na ndugu wa marehemu yameongozwa na mkuu wa mkoa wa PWANI Bi MWANTUMU MAHIZA pamoja na wabunge na viongozi wa dini.


Akisoma risala yake Mkuu wa mkoa Pwani Bi MWANTUMU MAHIZA ameliagiza jeshi la polisi kumkamata dereva wa basi hilo na ikishindikana kukamatwa mara moja akamatwe mmiliki wa basi hilo na familia yake.

No comments:

Post a Comment