Tuesday, June 14, 2011

WATENDAJI IDARA YA MAHAKAMA SHINYANGA WASHIKILIWA NA POLISI KWA UBAKAJI!

Watu watatu wakiwemo wafanyakazi wa Idara ya Mahakama na Idara ya Afya katika halmashauri ya wilaya ya Meatu wanashikiliwa na polisi wilayani humo kwa tuhuma za kubaka na kupora shilingi elfu arobaini kwa binti mmoja ambaye ni mfanyakazi wa Baa moja iliyoko mjini Mwanhuzi.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Shinyanga JUSTUS KAMUGISHA amesema Watu hao walimbaka binti huyo mwenye umri wa miaka 21(jina limehifadhiwa) mkazi wa eneo la Mshikamano mjini hapa juni 09, mwaka huu majira ya saa 4.30 usiku kando kando ya barabara ya Mwanhuzi kuelekea Mwambiti.
Kamanda KAMUGISHA ametaja majina ya Watumiwa hao kuwa ni pamoja na EMANUEL MAGULYATI maarufu kwa jina la NHANDI, mlinzi wa mahakama ya wilaya ya Meatu, JUMA JENGUO dereva wa idara ya Afya katika halmashauri hiyo, pamoja na KABWEBWE DAUDI mfanyabishara ndogondogo katika soko kuu la mjini Mwanhuzi.
Ameongeza kuwa Jeshi la Polisi Wilayani humo litafuatilia kwa ukaribu tukio hilo la kinyama ambayo yameanza kukithiri katika maeneo mbalimbli mkoani Shinyanga.

No comments:

Post a Comment