Thursday, August 4, 2011

SHEIKH MKUU MUFTI SIMBA AVUNJA JUMUIYA YA WANAWAKE WAISLAM!

Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti ISSA SHAABAN SIMBA ameivunja Jumuiya ya Wanawake wa Kiislamu BAKWATA na kuunda jumuiya mpya ya muda kwa lengo la kuandaa na kuratibu shughuli zote za wanawake wa Kiislamu.

Akitangaza maamuzi hayo jijini Dar es Salaam Sheikh Mkuu Mufti SIMBA amemtangaza Mwenyekiti mpya wa Jumuiya hiyo kuwa ni Bi SHAMIM KHAN na kutumia fursa hiyo kuwasisitiza wanawake wote wa Kiislamu kushikamana na kupeana mbinu mbalimbali za kujikomboa kimaisha


Kwa upande wake BI SHAMIM aliahidi kushughulikia majukumu yote ya Jumuiya hiyo ikiwemo kuibua changamoto zinazowakabili wanawake wa kiislam nchini.

No comments:

Post a Comment