Thursday, August 4, 2011

MBOWE AWAOMBA WABUNGE WAUNGANE KUIPINGA BAJETI YA UCHUKUZI!

Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni Mheshimiwa FREEMAN MBOWE amewaomba Wabunge wote wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania bila kujali itikadi zao za kisiasa kutopitisha Bajeti ya Wizara ya Uchukuzi ili kuliondolea taifa aibu ya kukosekana kwa huduma ya usafiri kwa njia ya Reli na Ndege.

Akichangia Bajeti ya Wizara ya Uchukuzi Mheshimiwa MBOWE amesema ili nchi ikabiliane na ushindani wa kimaendeleo na mataifa jirani wabunge hawana budi kuchukua hatua hiyo kwa kuipa changamoto serikali ikajipange upya katika kuliondoa taifa kwenye umaskini.


Serikali tayari imekiri ubia kati yake na Kampuni ya Rites Consortium ya India uliounda Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) haukuwa na tija na kuamua kusitisha mkataba wake na kulirudisha chini ya uendeshaji wa serikali kwa asilimia mia.

No comments:

Post a Comment