Thursday, August 4, 2011

TANZANIA BADO YAKABILIWA NA CHANGAMOTO YA UTAPIAMLO!

Imeelezwa kuwa bado Tanzania inakabiliwa na changamoto ya tatizo la utapiamlo ambao umekuwa ukipunguza kasi ya maendeleo ya tanzania katika ukuzaji wa uchumi na upunguzaji wa umasikini, na kwamba hali hiyo inapunguza utendaji wa watoto mashuleni na kupunguza tija ya kazi wanapokuwa watu wazima.

Katika kuendeleza jitihada za kupambana na utapia mlo, taasisi mbalimbali zimeanzisha ubia kwa ajili ya lishe Tanzania unaojulikana kama PANITA na kuweka wazi utekelezaji wa mipango na mkakati wa taifa wa lishe na sera nyingine mbadala.


Meneja wa PANITA, Bwana JOSEPH MUGYABUSO, amebainisha kuwa watoto 130 wenye umri chini ya miaka mitano nchini hupoteza maisha kila siku kutokana na ukosefu wa lishe bora huku tatizo la utapiamlo sugu likizidi kuwa kubwa ambapo asilimia 42 ya watoto wenye umri huo wamedumaa kutokana na tatizo hilo.


Mpango huo wa ubia unatarajiwa kuzinduliwa rasmi kesho na waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Prof. JUMANNE MAGHEMBE.

No comments:

Post a Comment