Wednesday, November 23, 2011

VIJANA WAPINGA AMANI KUWATAJA VIONGOZI WA DINI WANAOJIHUSISHA NA SIASA!

                              AGUSTINO MATEFU - Mwanasheria wa Kamati ya Vijana
Kamati ya Vijana Wapenda Amani nchini imelaani makundi mbalimbali kufanya maandamano yasiyo na tija kwa taifa na hivyo kuliomba Jeshi la Polisi nchini kitengo cha intelejensia kufanya uchunguzi wa kina kabla ya maandamano yoyote kuruhusiwa.

Katibu Mkuu wa kamati ya Vijana CHIFU MSOPA amesema kuelekea mchakato wa uundwaji wa katiba mpya serikali haina budi kuchunguza maandamano yoyote yanayoitishwa na vyama vya siasa, taasisi, wanaharakati na wanafunzi wa vyuo vikuu kwani yanaweza kuhatarisha amani.


Naye Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Vijana wapenda amani SAID MWAIPOPO ametumia fursa hiyo kuwaomba baadhi ya viongozi wa dini wanaorubuniwa kwa fedha ili kuvuruga amani kuacha vitendo hivyo mara moja vinginevyo kamati yake itawataja hadharani.

No comments:

Post a Comment