Tuesday, July 5, 2011

BALOZI WA UJERUMANI DK GUIDO HERZ AMUAGA MAKAMU WA RAIS!

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Dkt. Guido Herz, wakati alipofika ofisini kwake Ikulu Dar es Salaam leo Julai 04, 2011 kwa ajili ya kumuaga rasmi baada ya kumaliza muda wake nchini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Dkt. Guido Herz, wakati alipofika ofisini kwake Ikulu Dar es Salaam leo Julai 04, 2011 kwa ajili ya kumuaga rasmi baada ya kumaliza muda wake nchini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Finland nchini Tanzania, Juhan Toivonen , wakati alipofika ofisini kwake Ikulu Dar es Salaam leo Julai 04, 2011 kwa ajili ya kumuaga rasmi baada ya kumaliza muda wake nchini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya kitabu kutoka kwa Balozi wa Finland nchini Tanzania, Juhan Toivonen , wakati alipofika ofisini kwake Ikulu Dar es Salaam leo Julai 04, 2011 kwa ajili ya kumuaga rasmi baada ya kumaliza muda wake nchini. Picha Zote na Muhidin Sufiani-OMR

MABALOZI WA FINLAND NA GERMANY WAMUAGA MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, DKT. MOHAMMED GHARIB BILAL IKULU LEO JUMATATU JULAI 04, 2011

Mabalozi wa nchi za Finland na Ujerumani leo wamefanya ziara katika ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikulu jijini Dar es Salaam kwa lengo la kumuaga huku kwa pamoja wakielezea kubakia na kumbukumbu ya namna Watanzania wanavyoishi na walivyowathamini wakati wakifanya kazi za kidiplomasia hapa nchini.


Wa kwanza kufika ofisini kwa Makamu wa Rais alikuwa Balozi Juhan Toivonen kutoka Finland ambaye aliisifia Tanzania na kumzawadia Makamu wa Rais Kitabu cha “The Great Savanna” kitabu kilicho na vivutio kadhaa vya utalii nchini Tanzania ambacho kilichapishwa kwa Kifini na kisha kutafriwa kwa Kiingereza. Balozi huyo alimuahidi kutoa kopi nyingine za kitabu hicho zipatazo 9,000 kwa Makamu wa Rais ili zisambazwe kwa wadau wa utalii nchini.

Kwa upande wake Makamu wa Rais licha ya kumshukuru Balozi Toivonen, alifafanua kuwa uhusiano wa Finland na Tanzania ni wa siku nyingi na wenye tija nchini na kwamba historia inaonyesha kuwa katika fani ya Jiolojia, nchi ya Finland imesaidia sana katika kutanua rasilimali watu hapa nchini.


Katika hatua nyingine Balozi huyo alitaka kujua namna Tanzania inavyomudu kutanua demokrasia kulinganisha na mataifa mengine ya Afrika na Makamu wa Rais akamjibu kuwa, hali hii inatokana na mahusiano chanya kati ya serikali na wananchi na akatilia mkazo juu ya uongozi uliotukuka wa Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere hasa katika vigezo vya kujenga ushirikiano na hali ya kukubaliana kama Watanzania.

No comments:

Post a Comment