Wednesday, November 23, 2011

WANAOISHI PEMBEZONI MGODI WA ALMASI WIILIAMSON SHINYANGA WATAHADHARISHWA NA BARUTI!

                                                   Almasi kutoka mgodi wa Williamson
Wananchi wanaoishi pembezoni mwa mgodi wa Almasi wa WILLIAMSON Wilayanii Kishapu Mkoani Shinyanga wametahadharishwa kuacha kupita katika maeneo wanayopiga baruti kutokana na athari mbalimbali zinazoweza kutokea ikiwemo ulemavu wa kudumu au kifo.

Akitoa maelezo ya namna kwa mkuu wa mkoa wa shinyanga, ALLY RUFUNGA, juu ya namna wanavyopiga baruti mmoja wa watumishi wa mgodi huo Bw Donatus Makungu amesema kuwa wakati wa kupiga baruti mawe yanaruka juu sana na kwamba jitihada zinaendelea kuwatahadharisha wananchi.


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga yupo Wilayani Kishapu kwa ziara yake ya kikazi ya kukagua na kuona shughuli mbalimbali zinazofanyika ikiwa pamoja na kutoa melekezo kwa watumishi na watendaji.
                                   Huu ni moja ya mtambo mgodi wa Almasi wa WILLIAMSON.

No comments:

Post a Comment