Tanzania inatarajia kuungana na nchi nyingine kote duniani kuadhimisha siku ya ukatili wa kijinsia ambayo hujulikana kama siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kuanzia Novemba 26 hadi Desemba 10 kila mwaka.
Nchini Tanzania vitendo vya ukatili wa kijinsia vimekuwa vikiongezeka kwa kasi kubwa, ambapo unyanyasaji huo umejitokeza katika sura mbalimbali ikiwemo vipigo, ukeketaji ubakaji, mauaji ya wanawake na watoto, kurithi wajane na ukatili nyumbani.
Mkurugenzi wa chama cha waandishi wa habari wanawake TAMWA, Bi Annanilea Nkya, ametoa wito kwa vyombo vya habari wakati wa mkutano wake na wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari kuyapa kipaumbele na kuyakemea matukio ya unyanyasaji wa kijinsia kuanzia ngazi ya familia, mtaa, kijiji, na hatimaye taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake Dokta KANTANTA SIMWANZA, kutoka mradi wa Champion, anaweka wazi namna ukatili wa jinsia unavyoathiri jamii hasa wanawake na watoto.
No comments:
Post a Comment