Kituo cha Sheria na haki za binadamu ( LHRC), kimeelezea mapungufu yaliyojitokeza katika Uchaguzi mdogo wa Igunga ikiwemo idadi kubwa ya watu wasiojua kusoma na kuandika huku baadhi ya wakazi jimboni humo wakiuza shahada zao za kupigia kura baada ya kushawishiwa na baadhi ya watu waliosadikika kuwa wafuasi wa vyama vilivyoshiriki katika uchaguzi huo.
Hayo yamebainishwa hii leo, Jijini Dar es salaam, katika taarifa ya awali juu ya uchaguzi mdogo wa Igunga baada ya uchunguzi mdogo uliofanywa na Kituo hicho kwa kushirikiana na Asasi za kiraia zinazounda mtandao wa uangalizi wa ndani katika Uchaguzi (TACCEO).
No comments:
Post a Comment