Thursday, July 14, 2011

SERIKALI YALIA NA MALALAMIKO YA WANAFUNZI BODI YA MIKOPO!

                                                       DK SHUKURU KAWAMBWA
Serikali imesema licha ya jitihada zote inazofanya katika kuboresha upatikanaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu nchini, Ripoti iliyotolewa na Tume maalum ya Rais ya kuangalia matatizo yanayoikabili bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu inaonesha kuwa bado kuna malalamiko kuwa mikopo hiyo haitoshi.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi DK SHUKURU KAWAMBWA amesema mapendekezo yaliyotolewa na tume hiyo maalum ya rais pia yanaonesha kuwa jumla ya shilingi Bilioni 237 zilitengwa kwa ajili ya kutoa mikopo kwa wanafunzi 85,000.

Katika hatua nyingine Mheshimiwa KAWAMBWA amesema bodi hiyo haijafanya vizuri katika ukusanyaji na urejeshaji wa fedha zilizotolewa kwa mikopo ikilinganishwa na nchi nyingine Afrika ambapo mpaka sasa ni asilimia tatu tu ya fedha zilizotolewa kwa mikopo ndizo zilizorejeshwa.

No comments:

Post a Comment