Tuesday, November 29, 2011

WANANCHI WAOMBWA KUJITOKEZA MBIO ZA MWENGE DSM!

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam SAID MECK SADICK amewataka Wananchi kujitokeza kwa wingi katika kilele cha mbio za mwenge wa Uhuru, ambapo itakuwa ni mwanzo wa maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara,yatakayofanyika Disemba Mosi mwaka huu katika uwanja wa Uhuru hapa jijini.

Mkuu huyo wa mkoa wa DSM amesema baada ya Mwenge wa Uhuru kumaliza mbio zake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta JAKAYA KIKWETE ataupokea na kisha kuukabidhi kwa kikosi maalum, kitakachoanza safari ya kwenda kuupandisha katika mlima Kilimanjaro.


Mwenge wa Uhuru unapandishwa Mlima wa Kilimanjaro ili kuenzi siku ya Uhuru, ambapo Mwenge huo uliwashwa na kupandishwa kileleni kwa mara ya kwanza mwaka 1961.

No comments:

Post a Comment