HAMAD RAJAB TAO
Mtafaruku mkubwa umejitokeza kati ya viongozi na baadhi ya wanachama wa Tanzania Labour Party TLP kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari na Maelezo jijini Dar es Salaam wakati Naibu Katibu Mkuu (Utawala) HAMAD RAJAB TAO akizungumzia kauli iliyotolewa Mwenyekiti wa TLP Taifa AUGUSTINO LYATONGA MREMA kwamba viongozi wa chama hicho ni mzigo.
Hali hiyo ilichangiwa na baadhi ya wanachama wanaomuunga mkono MREMA kusambaza taarifa ndani ya ukumbi huo wakati mkutano ukiendelea iliyokuwa ikikanusha tamko alilokuwa akilitoa Naibu Katibu Mkuu TAO, kwamba wanachama wa chama hicho wanataka Mwenyekiti wa TLP Taifa ajiuzulu kwani anaizorotesha TLP.
Kwa upande wake BLANCA HAULE ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa TLP amepinga kitendo cha Mwenyekiti wao kuwa kiongozi wa kila idara ikiwemo msaini mkuu wa chama ambapo amesema suala hilo linachangia wanachama kushindwa kuhoji matumizi ya fedha ndani ya Chama hicho.
No comments:
Post a Comment