Tuesday, November 22, 2011

PROF TIBAIJUKA AIPONGEZA MAHAKAMA YA RUFAA KURUDISHA VIWANJA VYA WAZI VILIVYOKWAPULIWA NA KAHAMA MINNING KWA JAMII!

Serikali imepongeza maamuzi yaliyotolewa na mahakama ya rufaa kutupilia mbali hukumu ya mahakama kuu kuruhusu kampuni ya kibiashara ya Kahama mining co operation kumiliki sehemu ya viwanja vya wazi vilivyopo eneo la oysterbay wilaya ya kinondoni jijini Dar es Salaam.

Waziri wa ardhi,nyumba na maendeleo ya makazi PROFESA ANNA TIBAIJUKA amesema kuwa hukumu hiyo kimsingi itasaidia kuleta matumaini makubwa kwa wananchi ambao walikuwa na malengo ya kuyatumia maeneo hayo kwa matumizi ya kielimu, huku akizitaka kampuni binafsi kutotumia vibaya uwepo wa mahakama nchini kwa manufaa yao binafsi na kujaribu kuwanyima wananchi haki zao za msingi.

No comments:

Post a Comment