Tuesday, November 22, 2011

MOAT, JUKWAA LA WAHARIRI WAJADILI CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI!

Kufuatia tuhuma za ukiukwaji wa maadili na kutoa taarifa zinazochochea vurugu na uvunjifu wa amani unaofanywa na baadhi ya vyombo vya habari nchini Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya habari Tanzania MOAT kimekutana na Jukwaa la Wahariri Tanzania ili kujadiliana na kutoa maamuzi kuhusiana na tuhuma hizo.

Katika kikao hicho cha siku moja kilichoongozwa na Mwenyekiti wa MOAT Bw REGINALD MENGI, wahariri, na baadhi ya waandishi wa habari waandamizi wametoa maoni yao kuhusiana na vitendo vya baadhi ya waandishi wa habari kutoa maoni yao kwenye habari.

Baada ya majadiliano hayo kikao hicho kimetoa maazimio yake, na hapa Katibu Mtendaji wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya habari Tanzania HANRY MUHANIKA anayataja baadhi ya maazimio hayo.
             Baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari nchini wakiwa kwenye moja ya mikutano yao.

No comments:

Post a Comment