JESHI la polisi linawashikilia wakazi wawili wa mkoa Dodoma,kwa tuhuma za wizi wa mapipa 80 ya lami, yenye thamani ya zaidi ya Sh.Milioni 32,mali ya kampuni ya ujenzi wa barabara, Sinohydro Co-oparation ya nchini China.
Kaimu kamanda wa polisi mkoa Singida AYOUB TENGE amewataja watuhumiwa hao ni meneja wa kampuni ya Mtwiyira Traders, Peter Mtenga na msimamizi wa kampuni hiyo, Elivin Maedaeda.
Kamanda Tenge amesema , watuhumiwa hao waliiba mapipa hayo novemba 12 mwaka huu, saa kumi usiku, kwenye eneo la kambi ya kampuni hiyo inayojenga barabara ya lami,ya Singida-Katesh,mkoani Manyara.
Tenge amesema mapipa 74 yalikutwa ndani ya uzio wa kampuni ya watuhumiwa na mengine sita kwenye eneo la mradi, katika kijiji cha Chamwino, mkoani Dodoma.
No comments:
Post a Comment