Wednesday, November 23, 2011

VODACOM MEGA PROMO YAWANUFAISHA ZAIDI..!

Mega Promosheni inayoendeshwa na kampuni ya kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania imezidi kuchanja mbuga huku wananchi wakizidi kunufaika nayo kwa kushinda mamilioni ya shilingi pamoja na televisheni za kisasa aina ya Samsuing LCD.

Mwishoni mwa wiki Geoffrey Msitu mkazi wa Arusha aliingia katika orodha ya washindi wa kitita cha Shilingi Milioni Kumi na Moja, fedha ambazo kimsingi zitamsaidia kubadili maisha yake. Bw. Msitu pamoja na mshindi wa televisheni Bw.Godlove Mbise ambae nae ni mkazi wa Arusha walikabidhiwa zawadi zao mwishoni mwa wiki mjini Arusha na Mkurugenzi wa Vodacom Kanda ya Kaskazini Nguvu Kamando



Vodacom Mega Promosheni bado inaendelea na wateja wa Vodacom nchi nzima wanayo nafasi ya kushiriki na kujishindia mamilioni ya fedha kuboresha maisha yao.Ili kushirikli mteja wa Vodacom anapaswa kutuma neno BURE kwenda namba 15015.

No comments:

Post a Comment