Rais JAKAYA MRISHO KIKWETE, amepokea barua ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ya kuomba baadhi ya viongozi wa chama hicho kukutana naye kuzungumzia Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka huu.
Aidha Rais KIKWETE amesema amelipokea ombi hilo kwa kuwa ni jambo jema. Kufuatia kukubali kwake ombi hilo, Rais ameagiza mawasiliano yafanyike ili kupanga tarehe mwafaka ya kukutana na viongozi hao wa CHADEMA ili kuzungumzia suala hilo.
No comments:
Post a Comment