Baadhi ya wasamalia wema wakijitahidi kuokoa roho za watu ambao magari yao yamelaliwa na lori la mafuta.
Hapa kazi ya uokoaji ikiendelea, ndari ya gari hili jekundu abiria mmoja alitolewa akiwa mzima.
Waokoaji/wasamalia wema wakiwa kama hawaamini kilichotokea katika eneo hilo la Riverside. Huu ndio umati wa watu uliofika kushuhudia tukio hilo lililotokea majira ya saa mchana na kulifanya jiji la Dar es Salaam kuzizima kwa huzuni.
Watu watatu wamefariki Dunia huku wengine wanne wakijeruhiwa vibaya baada ya gari kubwa la mafuta Kampuni ya DELBIT, lenye namba T 269 BRQ kuacha njia na kugonga magari mengine saba yaliyokuwa kwenye foleni zikitokea Buguruni kuelekea Ubungo.
Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kinondoni, RPC CHARLES KENYELA, amesema ajali hiyo imetokea majira ya saa saba mchana katika barabara ya Mandela eneo la River Side, Jijini Dar es salaam na chanzo chake ni mwendo kasi wa lori la mafuta lililokuwa likitokea Ubungo Mataa kuelekea Buguruni.
Aidha kwa upande wa mashuhuda wa ajali hiyo wamesema chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa gari la mafuta alipojaribu kukwepa watu waliokuwa kwenye kituo cha daladala eneo la River Side na kuhamia upande wa pili wa barabara na kisha kuyagonga magari hayo.
No comments:
Post a Comment