Monday, October 24, 2011

UN LAJIPANGA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO ZILIZOPO BARANI AFRIKA IKIWEMO KUPUNGUZA VIFO VYA WATOTO!

                                 Waziri BERNARD MEMBE akizungumza na Wanahabari
Katika kuadhimisha miaka 66 ya Umoja wa mataifa duniani, Shirika hilo limejipanga kukabiliana na changamoto zilizopo barani Afrika ikiwemo kupunguza vifo vya watoto baada ya kuonekana kushika kasi ambapo imebainika zaidi ya watoto elfu 22 hufa kwa siku kwa sababu ya Umasikini.

Akizungumza katika siku ya Miaka 66 ya Umoja wa Mataifa iliyokuwa sambamba na ufungaji wa Maonyesho ya maadhimisho ya miaka 50 ya Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa yaliyofanyika jijini Dar es salaam katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa BERNARD MEMBE amesema changamoto kubwa ya Umoja wa Mataifa ni kuangalia jinsi ya kumlea mtoto katika dunia yenye watu bilioni 7 ili kuondokana na unyanyasaji wa watoto ambao ni kizazi kijacho.


Kwa upande wake Katibu Mkuu kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa Nchini, FANCY NKUHI ametoa wito kwa jamii kuamka na kuchukua hatua dhidi ya uvunjaji wa haki za wanawake.

No comments:

Post a Comment