Monday, August 29, 2011

WAKAZI JIJINI WATAKA WATENDAJI KUFANYA KAZI KWA KUWALETEA WANANCHI MAENDELEO!

Baadhi ya wakazi jijini Dar es Salaam wamewaomba watendaji wa Manispaa kote nchini kutekeleza majukumu yao kwa lengo la kuwaletea wananchi maendeleo tofauti na ilivyo sasa ambapo wamekuwa wakifanya kazi ili kuwaridhisha viongozi waliopo madarakani.


Wakizungumzia utekelezaji wa miradi ya barabara unaofanywa kwa ajili ya kupita mbio za Mwenge maeneo mbalimbali jijini wakazi hao wamesema barabara hizo hazitodumu kwani zinajengwa kwa zima moto na chini ya viwango vya ubora.

No comments:

Post a Comment