Monday, October 24, 2011

KAMATI YA BUNGE LA HESABU ZA MASHIRIKA YA UMMA IMEITAKA SERIKALI KUSITISHA KUPELEKA FEDHA BODI YA UTALII!

                                                                 Mh.Zitto Kabwe
Kamati ya Bunge ya Hesabu za mashirika ya Umma imeitaka Serikali kupitia Kamishna Mkuu wa fedha kusitisha kupeleka fedha kwenye Bodi ya Utalii kutokana na bodi hiyo kumaliza muda wake tangu mwaka 2009 huku ikiendelea kupatiwa fedha ambazo hazijulikani zimefanya kazi gani.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kikao cha kamati hiyo Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma Mhe. ZITTO KABWE amesema licha ya kamati hiyo kumaliza muda wake bado ilikuwa ikipata fedha kwaajili ya uendeshaji na kumtaka Waziri wa Maliasili na Utalii EZEKIEL MAIGE kukutana na kamati hiyo mwishoni mwa mwezi huu.


Naye kaimu mwenyekiti wa Bodi ya Utalii GEORGE LUBELEJE akizungumza na kituo hiki amekiri kuisha kwa muda wa kamati hiyo na kubainisha kuwa wao kama wanakamati wasingeweza kuchukua hatua zozote kutokana na jukumu la kuteua wajumbe wapya kuwa ni la Waziri wa Maliasili na Utalii.

No comments:

Post a Comment