Sunday, August 21, 2011

MSONDO YATWAA TUZO YA BEST RHUMBA GROUP KWA AFRIKA MASHARIKI!

BENDI ya muziki ya msondo ngoma imepata TUZO ya the Best Rhumba Group katika East Africa Music Awards mashindano yaliyofanyika Nairobi Kenya na kukusanyika kwa bendi za Afrika Mashariki na bendi ya Msondo kuibuka Kidedea katika mashindano hayo.

Akithibitisha ushindi huo Meneja wa Bendi hiyo Saidi Kibiriti amesema wameshinda tuzo hiyo na watahakikisha wanaionesha kwa mashabiki wa bendi hiyo ili kudhirisha kuwa bendi ipo ngangari popote duniani kutokana na kukamilika kila idara.

Bendi hiyo itanza mazoezi siku ya Jumatatu kwa ajili ya kujiandaa na sikukuu ya Iddi inayotarajia kufanyika wiki ijayo ambapo wanaingia kambini kusuka vibao vipya ikiwemo kuvifanyia kazi vile vya Zamani.

Aidha siku ya Iddi Mosi itapiga katika viwanja vya TTC Chang'ombe ambapo mashabiki watapata kuona tuzo hiyo ya Afrika Mashariki walioitwaa hivi karibuni na kupata fulsa ya kupiga nayo picha katika viwanja hivyo.Bendi hiyo inayotamba na vibao vyake vipya vya Suluu uliotungwa na Shabani Dede na Nadhiri ya Mapenzi uliotungwa na Juma Katundu.

No comments:

Post a Comment