Shirika la ndege la Ujerumani la Lufthansa limefuta safari za ndege 200 za kutua na kuondoka kutoka Frankfurt wakati wafanyakazi katika uwanja huo mkubwa kabisa nchini wakisema kwamba wanaingia tena kwenye mgomo.
Chama cha waongoza safari za ndege nchini GdF kimesema hapo jana kwamba wafanyakazi watagoma kwa masaa 48 kuanzia mapema leo hii.
Chama hiki kimekuwa kikishinikiza ongezeko la mishahara,kupunguzwa kwa masaa ya kazi na kutolewa kwa marupurupu makubwa kwa wafanyakazi wanaoongoza ndege kuingia na kutoka katika sehemu za kuegesha vyombo hivyo.
Migomo iliyofanyika Alhamisi na Ijumaa iliopita katika uwanja huo wa ndege wa Frankfurt ilisababisha kufutwa kwa safari za ndege 500.
No comments:
Post a Comment