Monday, October 24, 2011

BAADHI YA WAKAZI MAGOMENI KOTA WAANZA KUDHURUMIANA FEDHA ZA PANGO WALIZOLIPWA NA NHC!

Moja ya nyumba za NHC ambazo wapangaji wake wamelipwa ili wahame kupisha ujenzi wa nyumba za kisasa kwenye eneo hilo.

Na Theeastafrica Bloger
Mkazi wa Magomeni kota, Jijini Dar es salaam, EMANUEL PETER amedai kudhurumiwa na ndugu yake fedha taslimu shilingi milioni moja na laki moja iliyotolewa kwaajili ya fidia kwa wakazi wa eneo hilo kupisha ujenzi wa nyumba za kisasa.

Akizungumza na kituo hiki, Mkazi huyo amesema mara baada ya ndugu yake huyo kupokea fidia hiyo kutoka manispaa ya kinondoni ili kupisha zoezi hilo alianza kumsumbua kumpatia mgao wake na kutoweka usiku wa kuamkia leo.


Katika hatua nyingine baadhi ya Wakazi wa eneo hilo wameanza kuhama baada ya kulipwa fidia hiyo huku wengine wakisubiri malipo hayo kupisha zoezi hilo.
Moja ya nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa NHC iliyopo Upnga inavyoonekana baada ya kukarabatiwa!

No comments:

Post a Comment