Monday, August 1, 2011

CHEYO 'BWANA MAPESA' ASHAURI UONGOZI BODI YA PAMBA UWAJIBISHWE!


Chama cha united democratic party UDP, kimeitaka Serikali iuwajibishe uongozi wa Bodi ya Pamba kufuatia kushindwa kupanga bei halisi ya zao la pamba na kuwataka wakulima wa zao hilo kuendelea kupigania upatikanaji wa bei nzuri ya zao hilo itakayowafanya wamudu gharama za kilimo chake.

Akizungumza Jijini Dar es salaam, mapema hii leo Mwenyekiti wa Chama hicho, JOHN MOMOSE CHEYO, amesema Bodi hiyo imeshindwa kupanga bei halisi mbapo wakulima hukatwa shilingi 200 kama ushuru kwa kila kilo moja ya pamba, ambapo bei ya kilo moja ni kati ya shilingi 700 hadi 1300.

Aidha ameomngeza kuwa Serikali imekuwa ikiwashurutisha wakulima kuingia mikataba ya lazima bila kujua watanufaika vipi kupitia mikataba hiyo na kudai kuwa bodi ya Pamba nchini kwa sasa inaonekana kama wakala wa wanunuzi ambalo ni kosa kisheria.

No comments:

Post a Comment