Wednesday, July 20, 2011

WAKAANGA SAMAKI KUNDUCHI MTONGANI WALALAMIKIA USHURU WA SOKO!

Wakaanga Samaki katika soko la Kunduchi Beach Jijini DSM wameilalamikia Ofisi ya Serikali ya mtaa wa kunduchi mtongani kwa kuwatoza ushuru wa Shilingi 15,000 kila mwezi kwa ajili ya zoezi la usafi bila ya kuwepo kwa huduma hiyo.

Wamesema hawajawahi kufanyiwa usafi wa aina yote katika soko hilo bali wao wenyewe ndio wanaosafisha eneo lao huku ofisi ya mtendaji ikiendelea kuwatoza ushuru huo kila mwezi


Akijibu tuhuma hizo mwenyekiti mtendaji wa Serikali ya mtaa huo RICHARD RUSISYE amesema ushuru ambao wanaotozwa wakaanga Samaki hao ni makubaliano baina yao na Ofisi yake juu ya kuliweka eneo hilo katika hali ya usafi.

No comments:

Post a Comment