Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim SEIF SHARIFF HAMAD ameliagiza Shirika la Bandari pamoja na Idara ya Mazingira kumpa taarifa ya Kitalaam juu ya athari za ki-mazingira na maafa zinazoweza kutokea kutokana na ujenzi wa Hotel ya kitalii karibu na Bandari ya WESHA Visiwani humo.
Agizo hilo amelitoa wakati alipokutana naViongozi wa taasisi hizo pamoja na menejimenti ya hotel ya PEMBA MISALI COTTAGE ambapo amewataka wakabidhi ripoti hiyo katika kipindi cha muda usiozidi wiki sita kutoka Sasa.
Maalim SEIF amesema ameshtushwa na hatua ya ujenzi wa Hotel hiyo kwa sababu hali ya ki-mazingira katika eneo hilo siyo ya kuridhisha kwa kuwepo na Bandari pamoja na matenki ya mafuta yenye ujazo mkubwa, huku akibainisha kwamba hali hiyo ni hatari kwa maisha ya wananchi wataokuwa wakifika katika Hoteli hiyo.
Katika Hatua nyingine Maalim SEIF amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, iliyo katika mfumo wa Umoja wa Kitaifa, itaendelea kuendesha shughuli zake kwa kuzingatia kanuni na sheria zilizopo bila ya kumpendelea au kumuonea mtu yeyote visiwani humo.
No comments:
Post a Comment