Wednesday, July 20, 2011

USTAWI WA JAMII WAGOMA KUSHINIKIZA SERIKALI IBADILISHE UONGOZI!

Wanafunzi na Waalimu wa Taasisi ya Ustawi wa jamii wameendelea na mgomo,huku wakiulalamikia uongozi uliopo kwa kutokuwa na sifa zinazotakiwa na baraza la vyuo vya ufundi NACTE hali iliyopelekea kushindwa kufanya usajili wa wanafunzi kwa Mwaka wa 2011/12.

Wakizungumza na kituo hiki chuoni hapo baadhi ya wanafunzi wamesema mgomo unaoendelea umeathiri kwa kiasi kikubwa ratiba za masomo hivyo kushindwa kujua hatima ya mgogoro huo.


Hata hivyo kwa upande wa waalimu, Mhadhiri Msaidizi Idara ya Ustawi wa Jamii, Mariana Makuu amesema uamuzi wa kufikia hatua hiyo umetokana na Uongozi uliopo kuwafukuza baadhi ya walimu bila kufuata taratibu za Ki-sheria.


Aidha Kwa upande wa Uongozi kupitia kwa Mkurugenzi wa Mafunzo, ANDREW MCHONVU amesema tatizo la taasisi si tatizo la wanafunzi wote bali ni kwa kikundi kidogo cha baadhi ya waalimu ambao wamejaribu kuingiza jambo hili kwa wanafunzi ili kuitisha mgomo usiokuwa na tija. PICHA KWA HISANI YA FULLSHANGWE.

No comments:

Post a Comment