Thursday, July 14, 2011

UMOJA WA VIJANA WAZALENDO UDSM WAPANGA MAANDAMANO KUHAMASISHA ROSTAM AZIZ AFILISIWE MALI ZAKE!

Umoja wa vijana wazalendo wa vyuo vikuu DSM wameazimia kufanya maandamano endapo serikali haitachukua maamuzi ya haraka dhidi ya ROSTAM AZIZ aliyejiuzulu nafasi ya ubunge hapo jana, kwa kumpeleka mahakamani pamoja na kutaifisha mali zake zote.

Mwenyekiti wa umoja huo AGUSTINO MATEFU ambaye pia ni mjumbe wa mkutano mkuu wa mkoa wa DSM UVCCM amedai kuwa kujiuzulu kwa ROSTAM sio pigo la kisiasa bali ni wajibu wake kuwajibika kutokana na vitendo vyake vya kujaribu kuingiza serikali katika mazingira magumu.

No comments:

Post a Comment