Shirika la Umeme nchini ( TANESCO), limepokea Mtambo mpya wenye uwezo wa kuzalisha megawati 34 za umeme, kutoka Kampuni ya SIEMENS ya nchini Sweden wenye thamani ya Dolla milioni 120.
Afisa Uhusiano wa TANESCO, BADRA MASOUD, amesema mbali na mtambo huo wanatarajia kupokea mitambo mingine miwili ambayo itakamilisha idadi ya mitambo mitatu yenye uwezo wa kuzalisha megawati 100, itakayojengwa Ubungo Jijini Dsm na ujenzi wake ukitarajiwa kukamilika Desemba mwaka huu.
MASOUD ameongeza kuwa ili tatizo la mgao wa umeme unaoendelea nchini lipatiwe ufumbuzi wa kudumu na kubaki historia zinahitajika megawati za nyongeza 800 hadi 1000 za umeme.
No comments:
Post a Comment