Thursday, July 14, 2011

MSAMA AUCTION MART YAOMBA WABUNGE WAUNGE MKONO JUHUDI ZA KUKAMATA MAHARAMIA!

Wabunge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na wanaharakati wa haki za binadamu wameombwa kutoa ushirikiano kwa taasisi zinazolinda haki za wasanii wa Tanzania ikiwemo kudhibiti uharamia katika wizi wa kazi zao unaofanywa na wafanyabiashara wakubwa nchini.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Msama Auction Mart ALEX MSAMA amesema ili kuwakomboa wasanii wa Kitanzania wabunge kwa kushirikiana na wadau wengine hawana budi kuunga mkono jitihada hizo ili wasanii wanufaike na matunda ya kazi zao.


Ndani ya kipindi cha wiki mbili tayari Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na Kampuni ya Msama Auction Mart imewashakamata maharamia wawili wa kazi za wasanii kujibu tuhuma za kuhujumu kazi za wanamuziki.

No comments:

Post a Comment