Promota wa mpambano wa ngumi, Philemon Kyando 'Don King' akizungumza kuhusu mpambano wa Fransic Cheka na Kalama Nyilawila pichani kushoto Dar es salaam, wakati akiongea na wanahabari kuhusu mpambano huo utakaofanyika januar 28. (Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)
BONDIA Karama Nyilawila ameibuka na kudai kitendo cha kunyang'anywa mkanda wake wa ubingwa wa Dunia wa WBF, na waandaaji wa mashindano hayo hakimsumbui kwani yeye anachoaangalia ni maslay yake.
WBF jana ilitangaza kumnyang'anya ubingwa huo kupitia kwa wasimamizi wa pambano hilo hapa nchini Rais wa Shirikisho la ngumi za kulipwa Tanzania (PST) Emmanuel Mlundwa baada ya kutangaza kucheza pambano lisilo la ubingwa na Francis Cheka kitu ambacho hakikutakiwa na WBF.
Akizungumza Dar es Salaam leo, Nyilawila alisema, hawezi kucheza pambano kwa kutafuta sifa bila kuwa na fedha ya kujikwimu kimaisha kwani yeye anachoangalia zaidi ni maslahi. "Kunyang'anywa ubingwa hakunitishi kama historia ya kuwa bingwa wa Dunia wa WBF mwaka juzi itabaki kuwa pale pale ingawa wameninyang'anya mkanda bila kupigwa, mimi natafuta pesa sifa hazina nafasi kwangu kwani ubingwa wa Dunia naweza kuwania hata katika mikanda mingene kwa kuwa vyama vya mchezo wa ngumio viopo vingi Duniani ," alisema Nyilawila.
Alisema, amekaa kipindi kirefu bila kuwa na pesa na hata kupanda ulingoni sasa ameapata sehemu ya kujikwamua hawezi kuipoteza kwani hata pesa ambazo angezipata huko ni ndogo kuliko anazozipata katika pambano lake hilo na Cheka. Alisema, kwa sasa ameishapandisha uzito hadi kg 75 ambao amesaini kucheza na Cheka sasa ingemuia vigumu kushush haraka uzito huo hadi
kufikia kg 72 ambao alisaini katika ubingwa huo wa Dunia.
Aliongeza kuwa pambano lake na Cheka liko palepale na kwa sasa anaendelea kujifua na anaimani kumchapa hata wakifika raundi ya mwisho.Naye kwa upande wake Promota wa pambano hilo Philemon Kyando alisema, maandalizi yanaendelea ambapo mabondia wote wapoa katika hari ya kushindana ambapo litasimamiwa na TPBC.
Aliwataja mabondia watakaosindikiza pambano hilo kuwa ni Maneno Osward 'Mtambo wa gongo' akicheza na Nasib Ismail, Chaulembo Palasa na Seba Temba, Venance Mponji na Ibrahim Elask na Antony Mathias akiwa na Juma Afande. Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones na wengine kibao ‘DVD’ hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha Rajabu Mhamila ‘Super ‘D’.
“Ninatarajia kuwapelekea DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika pambano la Cheka na Maugo ili kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi,” alisema Super ‘D’.
No comments:
Post a Comment