Tuesday, July 19, 2011

BESIGYE: MUSEVENI ATAITUMBUKIZA UGANDA KATIKA SHIMO LA UMASIKINI


Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Dkt. Kizza Besigye amesema Rais Yoweri Museveni wa nchi hiyo amepoteza dira na huenda akaitumbukiza nchi katika shimo la umasikini. Matamshi ya Besigye ni radiamali kwa hatua ya Rais Museveni ya kumkingia kifua makamu wake wa zamani Profesa Gilbert Bukenya anayekabiliwa na tuhuma za ufisadi na ubadhirifu wa mali ya umma.


Rais Museveni alisema siku chache zilizopita kuwa Prof. Bukenya hana hatia na kwamba kesi inayoendelea kortini dhidi yake inapaswa kusimamishwa mara moja.


Kiongozi wa chama cha upinzani cha FDC aidha amekosoa madai ya Rais Museveni kwamba maandamano ya kutembea kwa miguu kwenda kazini yaliyokuwa yakiongozwa naye Dkt. Besigye ndiyo yaliyozidisha mfumuko wa bei za bidhaa muhimu. Kizza Besigye amesema madai hayo ya Museveni hayana msingi wowote.

No comments:

Post a Comment