Wednesday, July 20, 2011

MILIONI 221.5 ZATUMIKA KUNUNUA POWER TILLER WILAYA YA SINGIDA!

Zaidi ya Shilingi Milioni 221.5 zimegharamia manunuzi ya trekta kubwa tatu na Powertiller kumi, ili kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara, kwa Wananchi wa halmashauri ya Wilaya ya Singida.

Hayo yamebainishwa na afisa kilimo na mifugo Wilayani humo, AYOUB SENGO, kwenye taarifa aliyosoma mbele ya Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda, LAZARO NYALANDU, kwenye hafla fupi ya kukabidhi pembejeo hizo za kilimo.


Afisa kilimo na mifugo huyo amesema mpango huo umetumia asilimia 80 ya gharama zote za manunuzi ya trekta na powertiller hizo, wakati vikundi vya wakulimavikiwa vimechangia asilimia 20.


Kwa upande wake naibu waziri LAZARO NYALANDU amewataka wakulima wilayani Singida kuhakikisha kwamba wanaongeza uzalishaji wa mazao, ili kuondokana na tatizo la upungufu wa chakula hapa nchini.

NYALANDU ambaye ni mbunge wa Singida kaskazini,amesema mkakati wa Taifa wa Kilimo Kwanza ni lazima uende sanjari na ongezeko la fedha kupitia kilimo, ili makazi bora yapatikane badala ya kuishi katika nyumba za tembe.

No comments:

Post a Comment