Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto imekiri kuwa tatizo la watoto wa mitaani ni kubwa na linakuwa kila siku na jamii jamii haina budi kutoa ushirikiano ili kusaidia kulimaliza.
Naibu Waziri wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto UMMY MUYA amesema tathmini iliyofanywa na serikali mwaka jana kuangalia ukubwa wa tatizo la watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu imebaini kuwa tatizo hilo haliwezi kwisha bila familia kutoa mchango wake.
CHRISTINA LISSU Mbunge Viti Maalumu CHADEMA alimuuliza Naibu Waziri MUYA kama Serikali inafahamu idadi ya watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu na imepanga kuchukua hatua gani ili kuwasaidia.
No comments:
Post a Comment