Mkutano wa tano wa bunge la la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umeanza leo, ambapo katika kipindi cha maswali na majibu Serikali imewahakikishia wananchi kuwa imejipanga katika kuwalipa waalimu fedha za kujikimu kiasi cha sh.500,000 kila mmoja, kuboresha miundombinu, na kuwajengea makazi ya kuishi
Waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Dk Shukuru Kawambwa ameyasema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa jimbo la Muhambwe Mh. Felix Mkosamali, aliyetaka kujua serikali imejipangaje kuhakikisha inawawekea motisha waalimu ili wakubali kwenda kutumika vijijini, kwani wengi wao wanaendelea kung`ang`ania mjini.
Aidha amewataka waajiri kuondoa vikwazo dhidi ya waajiriwa wanaotaka kujiendeleza kimasomo, huku akiwataka waalimu waliomaliza masomo kutumikia katika nafasi zao kabla ya kuendelea na masomo ya ngazi nyingine ili wanafunzi wafaidi matunda ya elimu waliyoipata.
No comments:
Post a Comment