Sunday, March 25, 2012

MAJIMAREFU AWAKA KUUNGANISHWA NA NASSARI WA CHADEMA KATIKA PICHA ANAYODAI NI FEKI

"Picha hii nilipigwa nikiwa na huyu mbunge mwenzangu, Vicent Nyerere (kulia), lakini huyu wa kushoto (Joshua Nassari) hakuwepo karibu yangu kabisa! Yeye alikuwa mbali akiamrisha vijana wanichome moto tena akiwa na hasira, tofauti na anavyocheka katika picha hii. Huu ni mchezo mchafu wa kuunganisha picha kwenye kompyuta uliofanywa na CHADEMA na kwa makusudi gazeti hili likaichapisha, baada ya kuona kwamba hatua aliyofanya Nassari ya kutaka niuawe jana ni mbaya sana. Nitalishitaki gazeti hili". Analalamika Mbunge wa Korogwe Vijijini Stephen Ngonyani wakati akionyesha picha inayomuonyesha akiwa katika furaha ya hali ya juu yeye, Nyerere na Nassari. Picha hiyo imechapishwa jana ukurasa wa kwanza gazeti la Mwananchi.
Picha yenyewe anayolalamikia Profesa Majimarefu ndiyo hii kama ilivyonakiliwa kutoka gazeti la mwananchi.

No comments:

Post a Comment