Mama Salma Kikwete akiungana na baadhi ya Wachina wanaoishi nchini kuaga mwili wa BI HAN BING.
Na Theeastafrica Bloger.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa BENARD MEMBE ametoa salamu za rambirambi kwa familia ya Bi HAN BING aliyekuwa mhasibu wa jumuiya ya wafanyabiashara wa kichina Tanzania, ambaye alifariki Dunia siku tatu zilizopita kwa kupigwa risasi na majambazi maeneo ya KURASINI Jijini Dar es Salaam karibu na makao makuu yak Uhamiaji.
Akizungumza wakati wa kuaga mwili wa marehemu huyo tayari kwa mazishi, Waziri MEMBE amesema tukio kama hilo linaweza kumpata mtu yeyote bila kujali uraia wake na kuwataka Wachina kuwa wavumilivu na Serikali ya Tanzania itashirikiana nao katika kipindi hiki cha majonzi.
Hata hivyo jeshi la polisi nchini limewakamata watu watatu wanaosadikika kuhusika na tukio hilo. Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa maalum wa Dar es Salaam ACP SULEIMAN KOVA amesema tayari jeshi lake tayari linawashikilia watu watatu kuhusiana na tuhuma za mauaji ya BI HAN BING.
No comments:
Post a Comment