Thursday, June 16, 2011

TANZANIA KUONGOZA MKUTANO WA SITA WA KIMATAIFA WA UUNGANISHAJI WA MAWASILIANO MAENEO YA VIJIJINI!


Tanzania imechaguliwa kuwa mwenyeji wa Mkutano wa sita wa Kimataifa wa uunganishaji wa mawasiliano katika maeneo ya vijijini Afrika wenye lengo la kuhakikisha sekta ya teknolojia na mawasiliano TEKNOHAMA inasaidia kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwenye maeneo hayo.

Akifungua mkutano huo Katibu Mkuu wa Wizara ya Sayansi, Mawasiliano na Teknolojia, DK. FLORENS TURUKA amesema mkutano huo utakaohudhuriwa na washiriki kutoka Afrika na nchi zingine duniani utasaidia kuinufaisha Tanzania na rasilimali ilizonazo kupitia mawasiliano.
Kwa upande wake wake Mkurugenzi wa Mawasiliano Wizara ya Sayansi, Mawasiliano na Teknolojia CLARA ICHWEKELEZE amesema kufanyika kwa mkutano huo nchini kutasaidia wawekezaji watakaokuwa tayari kuwekeza katika sekta ya mawasiliano hasa vijijini.
Kauli Mbiu ya Mkutano huo utakaokuwa wa siku tatu itakuwa ‘ Mataifa yanashiriki vipi kuwaunganisha wananchi wanaoishi vijijini na Tekonolojia ya Habari na Mawasiliano’.

No comments:

Post a Comment