Tuesday, May 10, 2011

CHIKU GALAWA ATAKA WAGANGA WANAOBANDIKA MABANGO WAKAMATWE!

Mkuu wa Wilaya ya Temeke, CHIKU GALLAWA amemuagiza mkurugenzi wa Manispaa hiyo kuwakamata na kuwachukulia hatua za Kisheria Waganga wa kienyeji wanaokiuka agizo lake linalowataka kutobandika mabango ya matangazo yanayotangaza tiba za mapenzi na nguvu za kiume.

Akizungumza Jijini DSM na kituo hiki Bi GALLAWA amesema licha ya watendaji wake kuyaondoa baadhi ya mabango barabarani waganga hao wa kienyeji wamekuwa wakiyarudisha kwa kuyabandika tena jambo ambalo ni kinyume na maagizo aliyoyayotoa.
Katika hatua nyingine mkuu huyo wa wilaya amewashauri wananchi kutoamini vitendo vya Ushirikina na kudai kwamba hatua hiyo inachangiwa na hali ya Uvivu wa Kufikiri.

No comments:

Post a Comment