Serikali imekiri kukabiliwa na changamoto kubwa ya mpango uliopo wa kutoa mafunzo kwa walimu wengi zaidi ili kujaza nafasi za uhaba wa walimu unaozikabili shule za msingi na sekondari kwa lengo la kuleta uwiano kati ya walimu waliopo na idadi ya wanafunzi hapa nchini.
Akijibu maswali ya papo kwa papo Bungeni mjini Dodoma leo Waziri Mkuu MIZENGO PINGA amesema mbali na hilo pia waalimu wanakabiliwa na changamoto ya kuwa na hosteli na nyumba za kutosha kwa ajili ya kuwaweka walimu na wanafunzi katika shule husika.
Waziri Mkuu alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Iramba Magharibi Mwigulu Madelu aliyemuuliza kama serikali haioni umuhimu wa kuwakusanya wanafunzi wa tarafa moja kujisomea ndani ya eneo moja ili kukabiliana na upungufu wa walimu unaochangia matokeo mabaya wakati wa mitihani.
No comments:
Post a Comment