Mchungaji Mwandamizi wa Kanisa la Victory Christin Church VCC akishuhudia uzinduzi rasmi wa tukio la Campus Night 2011 linalotarajiwa kufanyika Novemba 11 mwaka huu.Wengine wanaoshuhudia ni baadhi ya wanavyuo waliohudhuria uzinduzi huo.
Hii ndio nembo rasmi ya tukio la Campus Night 2011 linavyoonekana baada ya kuzinduliwa leo jijini Dar es Salaam.
Mchungaji Mwandamizi wa Kanisa la Victory Christin Church VCC (Katikati) akizungumza na wanahabari mara baada ya kukamilika kwa hafla ya uzinduzi rasmi wa tukio la Campus Night 2011 linalotarajiwa kufanyika Novemba 11 mwaka huu.
Na Theeastafrica Bloger
Kanisa la Victory Christian Center ( VCC) Jijini Dar es salaa, limeazimia kuwaandaa Wanafunzi wa elimu ya juu nchini kimaadili pamoja na kuwajengea moyo wa Uzalendo kwa taifa lao Kufuatia kuporomoka kwa maadili kwa baadhi ya viongozi nchini.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa tukio linalofahamika kama CAMPUS NIGHT 2011, Jijini Dar es salaam, Mchungaji Mwandamizi wa Kanisa la Victory Christian Center, Dkt. HURUMA NKONE, amesema hatua hiyo itawawezesha vijana nchini kuwa na uwezo wa kuongoza katika Nyanja mbalimbli kitaifa na kimataifa.
No comments:
Post a Comment