Chama cha wabunifu Majengo Tanzania(AAT) kinatarajia kufanya maandamano kwa ajili ya kuishinikiza serikali kubatilisha vibali vya kuvunjwa kwa jengo la mahakama ya rufaa iliyopo katika mtaa wa Kivukoni Jijini DSM.
Rais wa chama hicho Msanifu majengo Bwana MBARAKA IGANGULA amesema maandamano hayo yanayotarajiwa kufanyika septemba 2 mwaka huu yameshinikiza pia wale wanaotaka kuwekeza katika jingo hilo kuacha mara moja na badakla yake watafute mahali pengine pasipo na hazina kama hiyo.
Bwana IGANGULA amesisitiza kuwa jengo hilo limebeba historia kwa Taifa na Tanzania kwa ujumla na linawakilisha historia ya ubunifu wa majengo tangu enzi za utawala wa ukoloni wa Mwingereza hivyo lazima sheria zilizowekwa kulinda historia ziheshimiwe.
No comments:
Post a Comment