SIASA

          SUDAN KUSINI NA KASKAZINI ZATAKIWA KUTATUA KERO ZISIZOTATULIWA
                                                      Wapiganaji wa Sudan ya Kusini
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetoa taarifa ya mwenyekiti, likihimiza pande za kusini na kaskazini mwa Sudan zitatue haraka iwezekanavyo masuala yote ambayo bado hayajatatuliwa, kabla ya Sudan Kusini ipate uhuru rasmi mwezi Julai mwaka huu.

Taarifa hiyo imesema, kutokana na kukaribia tarehe 9 mwezi Julai mwaka huu ambayo ni siku ya kumalizika kwa kipindi cha mpito cha "Makubaliano ya Amani kwa Pande zote" , baraza hilo linahimiza pande hizo zifanye mkutano wa ngazi ya juu zaidi, ili kufika makubaliano kuhusu masuala ambayo bado hayajatatuliwa kwenye "Makubaliano ya Amani kwa Pande zote" na suala kuhusu mpango baada ya kukwisha kwa muda wa makubaliano hayo.

                       UN YAHIMIZA MAZUNGUMZAO BAINA YA PALESTINA NA ISRAEL
Moja ya katuni inayoonesha madhara kutokana na mapigano kati ya Palestina na Israel
                                              Moja ya Mlipuko katika ukanda wa Gaza
Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia mambo ya siasa Bw. Lynn Pascoe, ameelezea wasiwasi wake kuhusu mazungumzo kati ya Palestina na Israel yanayoendelea kukwama, na amezihimiza pande hizo mbili zichukue hatua ili kuondoa hali hiyo.

Katika mkutano wa Baraza la usalama la umoja wa mataifa kuhusu suala la Mashariki ya Kati, Bw. Pascoe alisema, Palestina na Israel zinatakiwa kutambua kuwa mchakato wa siasa wa hivi sasa uko nyuma ikilinganishwa na maendeleo makubwa iliyopata mamlaka ya utawala wa Palestina katika kazi ya kuanzishwa kwa nchi ya Palestina. Kutokana na hali hiyo, ni muhimu kwa jumuiya ya kimataifa kuunga mkono na kuimarisha mamlaka hiyo, na kuhimiza pande hizo mbili kurudi katika mazungumzo.

    CHINA HAIKUBALI OPERESHENI YOYOTE LIBYA KUKIUKA MAAZIMIO YA UN
                                        Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon
China imeeleza msimamo wake wa kutokubali operesheni yoyote inayokiuka maazimio ya Umoja wa Mataifa. Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China ametoa kauli hiyo katika kujibu habari kuhusu Serikali ya Uingereza kutuma wataalamu 20 wa kijeshi kwenda Benghazi Libya inayodhibitiwa na kundi la upinzani.

Siku ya Ijumaa, rais Dmitry Medvedev wa Russia na Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban ki-moon walipokutana huko Moscow pia wamesisitiza kuwa wakati wa kutekeleza operesheni ya kijeshi iliyoidhinishwa na Umoja wa Mataifa, ni lazima kufuata kwa makini maazimio hayo.